1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Serikali yathibitisha watu 38 wameuwawa kwenye ajali ya ndege

5 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IN

Serikali ya jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imethibitisha kuwa idadi ya watu 38 wamekufa katika ajali ya ndege iliyotokea jana nchini humo.

Wizara inayohusika na maswala ya kibinadamu mjini Kinshasa imesema kwamba waliofariki ni pamoja na abiria 20 waliokuwa ndani ya ndege hiyo na wafanyakazi watatu.

Ndege hiyo ilianguka kwenye nyumba za watu muda mfupi tu ilipopaa kutoka mwenye uwanja wa kimataifa wa Ndjili.

Watu kumi na tano waliuwawa chini wakati ajali hiyo ilipotokea. Taarifa ya wizara ya maswala ya kibinadamu inaeleza kwamba takriban watu 30 wamejeruhiwa vibaya.

Uchunguzi umeanza mara moja kutathmini kilichosababisha ajali ya ndege hiyo aina ya Antonov 26 kutoka Urusi mali ya shirika la ndege la Africa One la nchini Kongo.

Ndege hiyo ilikuwa imekodishwa na kampuni ya Malila na ilikuwa inaelekea kusini mwa jimbo la Kasai.

Wafanyakazi watatu katika ndege hiyo walikuwa raia wa Ukraine.