KINSHASA:Rais Kabila afanyia mabadiliko jeshi lake | Habari za Ulimwengu | DW | 13.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA:Rais Kabila afanyia mabadiliko jeshi lake

Rais Joseph Kabila amefanya mabadiliko katika uongozi wa jeshi lake.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotangazwa na televiesheni ya taifa mjini Kinshasa rais Kabila amemteua Luteni generali Diedonne Kayembe Mbandakulu kuwa mkuu wa majeshi yote akichukua mahala pa luteni generali Philemon Kisempia Sungilanga.

Wataalamu wanasema orodha hiyo mpya jeshini inawajumuisha wale waliowatiifu kwa rais Kabila.

Bwana Diodonne mwenye umri wa miaka 6122 ni mzaliwa wa kusini mashariki mwa jimbo la Katanga ngome ya familia ya rais Kabila.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com