1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:MONUC na Jeshi la Kongo wapeleka walind amani Kivu ya kaskazini

31 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBU5

Jeshi nchini Kongo na Ujumbe wa Umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUC wamepeleka majeshi zaidi ili kudumisha usalama kwenye eneo la mashariki baada ya mapigano kutokea hapo jana.

Helikopta mbili za Umoja wa mataifa zinazunguka mji wa Katale kwa lengo la kuwazuia wapiganaji kuanzisha tena ghasia.

Mapigano yalitokea hapo jana kati ya majeshi yanayomuunga mkono Kiongozi wa waasi Jenerali Laurent Nkunda na majeshi ya serikali mjini Katale ulio eneo la Masisi, Kivu ya Kaskazini.Yapata wanajeshi 30 wa serikali walijeruhiwa kwa mujibu wa msemaji wa jeshi Kanali Delhin Kahindi.

Mpaka sasa idadi kamili ya watu waliotoroka makazi yao kwenye kijiji hicho haijulikani japo wengine wanaripotiwa kuanza kurejea.

Eneo la mashariki ya Kongo linazongwa na mapigano kati ya wapiganaji,waasi vilevile jeshi la nchi hiyo.