1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA:Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa Kongo yatolewa

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCve

Kiongozi wa zamani wa Ghana Jerry Rawlings amesema kwamba nchi ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo haitopata nafasi nyingine endapo mpango wa sasa wa uchaguzi war ais utashindwa kufanikiwa.

Akizungumza mjini Kinshasa hapo jana Rawlings pia amewataka wakongomani kuondoa tofauti zao na kuiangalia nchi yao.

Katika ziara hiyo ya ujumbe wa Afrika nchini humo Rawlings aliandamana na kiongozi wa zamani wa Nigeria Abdulsalami Abubakar na marais wa zamani Pierre Buyoya wa Burundi na Sam Nujoma wa Namibia.

Wakati huo huo matokeo ya mwanzo katika duru ya pili ya uchaguzi huo war ais nchini Kongo yameonyesha ushindi war ais Kabila dhidi ya mpinzani wake bwana Jean Pierre Bemba.

Matokeo baada ya kuhesabiwa asilimia 5 ya masanduku ya kura yameonyesha rais Kabila ana asilimia 68.5 ya kura dhidi ya Bemba ambaye amepata asilimia 31.4.

Hata hivyo tume ya uchaguzi ya Kongo imesisitiza kwamba matokeo hayo sio rasmi na yanaweza kubadilika na kwamba matokeo kamili hayatarajiwi hadi Novemba 19.

Mshindi atatangazwa rasmi mwishoni mwa mwezi huu.