KINSHASA:Laurent Nkunda atoa mwito wa kusimamishwa mapigano | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA:Laurent Nkunda atoa mwito wa kusimamishwa mapigano

Kiongozi muasi jenerali Laurent Nkunda ametoa mwito wa kusimamishwa mapigano baada ya kuzuka upya mapigano katika jimbo la Kivu kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Zaidi ya wapiganaji 80 watiifu kwa jenerali Laurent Nkunda wameuwawa katika mapigano hayo.

Nkunda ametoa mwito huo wa kusimamishwa mapigano siku moja tu baada ya kutangaza kuwa amevunja makubaliano ya kusimamisha vita yaliyofikiwa kati yake na serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Jenerali muasi Laurent Nkunda amesema yuko tayari kuendeleza zoezi la kuwaunganisha wanajeshi watiifu kwa vikosi vya serikali kama ilivyoamariwa na serikali na umoja wa mataifa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com