1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa.Kabila amuamuru Bemba aondoke Kinshasa.

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCq6

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila amewapa walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo saa 48 kuondosha vikosi vinavyomtii mpinzani wake Jean-Pierre Bemba kutoka mji mkuu Kinshasa.

Kabila ambae ni mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi amesema, ikiwa Umoja wa Mataifa watashindwa kutekeleza agizo hilo, basi ataliamuru jeshi la Taifa liingilie kati.

Wasi wasi mkubwa umeenea katika mji Mkuu Kinshasa tangu wafuasi wa kiongozi wa zamani wa waasi Jean-Pierre Bemba walipozusha machafuko katika Korti kuu mjini humo.

Mshindani wa Rais Kabila bado anakataa kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa marudio uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.

Matokeo ya awali ya uchaguzi yaliyotangazwa yanaonyesha kuwa Joseph Kabila amejipatia asilimia 58.5.