KINSHASA:Ajali ya ndege yauwa watu watano | Habari za Ulimwengu | DW | 07.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA:Ajali ya ndege yauwa watu watano

Watu watano wameuwawa kufuatia ajali ya ndege ya mizigo katika eneo la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Gavana wa jimbo la Kivu ya Kaskazini Julien Mpaluku amefahamisha kwamba watu hao walifariki mara tu ndege yao ya mizigo ilipotuwa katika uwanja wa ndege wa Goma na kulipuka baada ya kugonga kigingi kilichokuwepo mahala hapo tangu mwaka 2001 kilichosababishwa na mkurupuko wa Volcano.

Watu wote watano waliofariki walikuwa raia wa Urusi.

Gavana Mpaluku amesema kwamba ndege hiyo ilitokea mjini Kinshasa na ilikuwa imebeba shehena ya mafuta na vipodozi.

Gavana huyo pia amefahamisha kuwa wanatafuta kujua iwapo ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria baada ya amri ya marufuku kwa ndege za mizigo kutolewa dhidi ya kuwapakia abiria hatua ambayo bado inakiukwa na kampuni kadhaa za ndege za mizigo katika eneo hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com