1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa: Watu wafariki kwenye ajali ya garimoshi nchini Kongo (Kinshasa)

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcq

Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kimetangaza watu kati ya 30 na arobaini wamefariki dunia kwenye ajali ya gari moshi.

Watu wengine kadha wamejeruhiwa katika ajali hiyo

Mabehewa kadha ya gari moshi hilo la usiku yanasemekana yalipinduka.

Gari moshi hilo lilikuwa linaelekea katika mji wa Kananga ambao ni mji mkuu wa jimbo la kusini la Kasai Magharibi.