KINSHASA: Watu 14 wauwawa mashariki mwa Kongo | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA: Watu 14 wauwawa mashariki mwa Kongo

Watu takriban 14 wameuwawa katika mapigano yaliyotokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Afisa wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo amesema waliouwawa ni wanamgambo 12 na wanajeshi wawili wa Kongo.

Msemaji wa umoja wa Mataifa mjini Bunia, Leocadio Salmeron, amesema mapigano yalizuka mnamo Jumapili iliyopita katika kijiji cha Singo, yapata kilomita 60 kusini mwa Bunia.

Jeshi la Kongo limeiambia tume ya Umoja wa Mataifa mjini Bunia kwamba wanajeshi wake saba wamejeruhiwa katika mapiganao hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com