1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Vikosi vya Ujerumani vimenza kuondoka Kongo

2 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnW
Hamid Karsai na Angela Merkel
Hamid Karsai na Angela MerkelPicha: AP

Ujerumani imeanza kuwarejesha nyumbani wanajeshi wake baada ya vikosi hivyo kukamilisha ujumbe wa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Kikundi cha kwanza cha wanajeshi 100 kinatazamiwa kuwasili leo hii katika uwanja wa ndege wa Cologne/Bonn.Serikali ya Ujerumani imesema,ujumbe huo uliokuwa sehemu ya tume ya amani ya Umoja wa Ulaya kulinda usalama wakati wa uchaguzi nchini Kongo,umefanikiwa.Wakati huo huo,kamanda wa vikosi hivyo nchini Kongo,Jemadari Christian Damay wa Ufaransa amesema,vikosi vya amani vya Umoja wa Ulaya vimechukua hatua ya kwanza ya uwezekano wa kuwa na jeshi la pamoja.Hii ni mara ya kwanza kwa Umoja wa Ulaya kupanga na kuongoza tume ya aina hiyo.Wanajeshi kutoka nchi 17 za Umoja wa Ulaya na Uturuki walishirikiana kuvisaidia vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa.