Kinshasa. Upigaji kura unaendelea vizuri. . | Habari za Ulimwengu | DW | 29.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kinshasa. Upigaji kura unaendelea vizuri. .

Upigaji kura unaendelea katika uchaguzi wa duru ya pili wa rais katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Upigaji kura umekuwa wa amani kwa kiasi kikubwa hadi sasa, hata hivyo umoja wa mataifa umesema kuwa mtu mmoja ameuwawa katika mji wa kaskazini mashariki wa Bumba.

Kura hiyo inawapambanisha rais Joseph Kabila dhidi ya kiongozi wa zamani wa waasi Jean Pierre Bemba, huku wagombea wote wakiahidi kutekeleza sheria za uchaguzi.

Pia wamewataka waungaji mkono wao kuwa watulivu baada ya kiasi watu 23 kuuwawa katika mapigano ambayo yalifuatia uchaguzi wa duru ya kwanza hapo Julai 30.

Uchaguzi huo wa duru ya pili utakamilisha uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasi nchini humo katika muda wa miaka 40.

Upigaji kura unaangaliwa na zaidi ya wachunguzi wa kimataifa wapatao 1,000, pamoja na jeshi la kulinda amani la umoja wa Ulaya ukiwa chini ya uongozi wa Ujerumani.

Matokeo hayatarajiwi hadi baada ya wiki kadha.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com