1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Ujumbe wa umoja wa mataifa wavurumishiwa mawe.

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwk

Makundi ya watu waliokuwa wakirusha mawe yamesababisha kwa siku ya pili jana kurejea kwa kundi la ujumbe wa umoja wa mataifa , uliotumwa kuchunguza mauaji ya karibu wanavijiji 18 , mauaji yaliyofanywa na watu wanaosadikiwa kuwa ni waasi wa Rwanda mashariki ya Kongo, DRC.

Maafisa wa umoja wa mataifa wamesema kuwa kundi hilo la ujumbe wa umoja wa mataifa , ulikuwa unajaribu kufika katika vijiji vitatu katika jimbo lenye matatizo la Kivu ambapo wanavijiji walikuwa wamelala walipigwa marungu ama kukatwa mapanga hadi kufa katika shambulio ambalo lilianza usiku wa Jumamosi.

Watu zaidi ya 12 wametekwa nyara na wengine 23 wamejeruhiwa katika tukio hilo, lililotokea katika eneo la Kanyola, kilometa 50 magharibi ya mji mkuu wa jimbo hilo Bukavu.

Kwa mujibu wa ujumbe ulioachwa baada ya tukio hilo la mauaji , kikundi cha waasi wa Rwanda , the Democratic Forces for the Liberation of Rwanda FDLR , kimefanya mauaji hayo kwa kulipiza kisasi kutokana na operesheni za jeshi la Kongo dhidi ya kundi hilo.