1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Makubaliano kusitisha mapigano Kongo

7 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSC

Makubaliano yamepatikana,kusitisha mapigano kati ya majeshi ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na vikosi vya jemadari muasi,Laurent Nkunda.Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Kongo, imesema,ilisimamia makubaliano hayo katika mji wa Sake ulio mashariki mwa nchi.Mapigano katika eneo hilo,yamesababisha zaidi ya watu 200,000 kukimbia makwao tangu mwanzoni mwa mwaka huu.