KINSHASA: Bemba aenda Ureno | Habari za Ulimwengu | DW | 11.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA: Bemba aenda Ureno

Kiongozi wa zamani wa waasi nchini Jamhuri ya kidemkorasia ya Kongo, Jean Pierre Bemba, ameondoka leo kwenda nchini Ureno kwa matibabu kutumia ndege ya kibinafsi.

Bemba, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Kongo, amekuwa akijificha kwenye ubalozi wa Afrika Kusini kwa majuma matatu baada ya vikosi vyake kuchakazwa na wanajeshi wa serikali katika siku mbili za mapigano makali mjini Kinshasa mwezi uliopita.

Ureno imempa ruhusa Jean Piere Bemba pamoja familia yake kuingia nchini humo ili mradi hatajihusisha na siasa akiwa ndani ya nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com