1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINGSTON : Kocha wa Pakistan hakuuliwa

Polisi ya Jamaica imefuta uwezekano kwamba kifo cha kocha wa zamani wa kriket wa timu ya Pakistan Bobb Woolmer kimetokana na mauaji.

Polisi awali ilisema kwamba Woolmer alikufa baada ya kunyongwa.Woolmer mwenye umri wa miaka 58 alikufa ikiwa ni siku moja tu baada ya Pakistan kutolewa na Ireland bila ya kutarajia katika Michuano ya Kriket Kombe la Dunia iliokuwa ikifanyika Jamaica.

Kundi la siri la majambazi linalojishughulisha na kamari lililaumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Kamishna wa polisi wa Jamaica Lucius Thomas amesema kwamba ushahidi mpya kutoka kwa waatalamu wa magonjwa na sumu umethibitisha kwamba uovu haukuhusika katika kifo chake.

Polisi hiyo ya Jamaica sasa imeifunga kesi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com