1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Olga kinaelekea Kuba

13 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Caz6

SANTO DOMINGO:

Hadi watu 14 wamepoteza maisha yao katika kimbunga kilichopiga eneo la Karibea.Watu wengi pia wanakosekana.Hasa ni eneo la kaskazini ya Jamhuri ya Dominik lililoathirika vibaya zaidi. Mvua kubwa zilizonyesha,zimesababisha mafuriko kwenye mto wa Yaque na katika mji wa Santiago. Kimbunga hicho kikiitwa OLGA sasa kinaelekea Kuba lakini kimepunguka nguvu.