1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Dunia la Rugby laingia nusu fainali

19 Oktoba 2015

Michuano ya Kombe la Dunia la mchezo wa Rugby imeingia nusu fainali. Argentina na Australia zilipata ushindi na kukamilisha hatua ya robo fainali hapo jana

https://p.dw.com/p/1GqYD
Rugby Tackle Verletzungen Sport Mannschaftssport
Picha: Getty Images/M.Runnacles

Ireland, ambayo haijawahi kufika katika nusu fainali ya Kombe la Dunia, na Scotland, ambayo ilifika nne bora mwaka wa 1991, zitalazimika kusubiri tena kwa miaka mingine minne.

Ireland walinyamazishwa na Argentina 43 kwa 20 mjini Cardiff. Scotland ilivunjwa moyo baada ya kuondolewa na Australia 35-34 ushindi uliopatikana kutokana na penalty ya dakika ya mwisho. Isipokuwa icha za video zinaonyesha kuwa penalti hiyo haikustahili.

Argentina hivyo basi watashuka dimbani Jumapili dhidi ya Australia katika nusu fainali ya pili. Nusu fainali ya kwanza itakuwa kati ya watani wakali wa tangu jadi New Zealand na Afrika Kusini siku ya Jumamosi.

New Zealand iliwabomoa Ufaransa 62-13 wakati Afrika Kusini wakiwazidi nguvu Wales 23 – 19.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu