1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI : Ufaransa yachunguzwa kwa mauaji ya kimbari

25 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzW

Rwanda inachunguza madai kwamba wanajeshi wa Ufaransa waliwaunga mkono wanamgambo ambao waliendesha mauaji ya kimbari katika kipindi cha miezi mitatu hapo mwaka 1994.

Rais Paul Kagame wa nchi hiyo ambaye ni wa kabila la Watusi na ambaye serikali yake imeingia madarakani baada ya mauaji hayo ya kimbari ameishutumu Ufaransa kwa kuwapatia mafunzo na silaha wapiganaji wa kabila la Wahutu ambao walikuwa wahusika wakuu katika mauaji ya siku 100 ambapo kwayo Watutsi 800,000 na Wahutu wa msimamo wa wastani waliuwawa.

Maafisa wanasema tume ya watu saba itasikiliza ushahidi kutoka kwa watu 20 katika kipindi cha wiki moja ijayo ambao utatumiwa kama ni ushahidi katika hatua ya kisheria itakayochukuliwa na serikali ya Kigali dhidi ya Ufaransa.

Kamati ya bunge ya Ufaransa hapo mwaka 1998 imesema kwamba nchi hiyo haikuhusika na mauaji hayo ya halaiki lakini imekiri kwamba yalifanyika makosa makubwa.