1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Rwanda imevunja uhusiano wa kibalozi na Ufaransa

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpb

Rwanda imevunja uhusiano wake wa kibalozi na Ufaransa.Waziri wa kigeni wa Rwanda,Charles Murigande alipozungumza mjini Kigali,alisema balozi wa Ufaransa amepewa saa 24 kuondoka Rwanda.Hatua hiyo imechukuliwa baada ya jaji wa Ufaransa kusema kuwa Rais Paul Kagame na washirika wake 9 wanapaswa kushtakiwa kuhusu kifo cha rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana. Siku ya Jumatano,jaji Jean Louis Bruguiere alitoa waranti za kuwakamata maafisa 9 wa Rwanda kwa tuhuma za mauaji yaliotokea baada ya kuangushwa kwa ndege ya rais wa zamani Juvenal Habyarimana aliekuwa Mhutu.Jaji huyo amesema dhima ya Kagame katika ajali hiyo yapaswa kuchunguzwa pia.Kagame amekanusha madai hayo na kusema kuwa tuhuma hizo zina sababu za kisiasa.Ajali hiyo ya ndege mwaka 1994 ilichochea mauaji ya maelfu ya Watutsi na Wahutu waliokuwa na msimamo wa wastani.