1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Mtawa ameadhibiwa kifungo cha miaka 30

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtv

Mtawa wa Kirwanda alietuhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda amekutikana na hatia na amepewa kifungo cha miaka 30.Sista Marie Theophista Makurabibi alikutikana na hatia katika mahakama ya wananchi ya kijijini kusini mwa mji wa Huye.Yeye ni mtawa wa kwanza kuhukumiwa kwenye mahakama ya Rwanda katika kesi ya kuhusika na mauaji ya halaiki ingawa mahakama nchini Ubeligiji imewahukumu watawa wawili kwa dhima yao katika mauaji yaliotokea kwenye shule, kusini mwa Rwanda.Kiasi ya watu 80,000,hasa Watutsi walio wachache na Wahutu wenye siasa za wastani waliuawa na Wahutu wa siasa kali katika mauaji ya siku 100 kati ya mwezi April na Julai.