Kifungo cha miaka 20 kwa Meja wa zamani wa Rwanda
6 Julai 2007Matangazo
Adhabu hiyo imetolewa kwa mauaji ya wanajeshi 10 wa Kibeligiji yaliyotokea mwaka 1994.Wanajeshi hao wa Kibeligiji walikuwa sehemu ya vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa na waliuawa siku moja baada ya ndege ya rais wa Rwanda kuangushwa tarehe 6 mwezi wa Aprili mwaka 1994.Kufuatia mauaji ya wanajeshi hao wa Kibeligiji,Umoja wa Mataifa uliondoa vikosi vyake kutoka Rwanda.Katika mauaji yaliyofuata,kiasi ya watu 800,000 waliuawa na Wahutu wenye siasa kali. Wengi waliouawa,walikuwa wa kabila la wachache la Watutsi na pia Wahutu wa siasa za wastani.