1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEW: Kinyangányiro cha madaraka kinaendelea Ukraine

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByO

Mgogoro wa kisiasa ukiendelea nchini Ukraine,Rais Viktor Yushchenko ametoa amri ya kuviweka vikosi vya wizara ya ndani,chini ya udhibiti wake. Taarifa ya serikali imesema,hatua hiyo imepaswa kuchukuliwa kwa usalama wa nchi.Siku ya Alkhamisi,Rais Yushchenko alimfukuza kazi mwendesha mashtaka alie mashuhuri nchini humo, Svyatoslav Piskun.Waziri wa ndani,Vasyl Tsushko akaviamuru vikosi vya polisi vinavyouzuia ghasia kuidhibiti ofisi ya Piskun.Baadae,Yushchenko alimtuhumu Tsushko kuwa amevunja sheria.Tsushko anajulikana kuelemea upande wa Waziri Mkuu Viktor Yanukovich,ambae tangu miezi kadhaa anajikuta katika kinyangayiro cha madaraka na Yushchenko.