1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV:Yushchenko ataka uchunguzi kuhusiana na uhesabuji kura

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKs

Rais Viktor Yushchenko ametaka kuwepo uchunguzi kuhusiana na uhesabuji kura kufuatia uchaguzi mkuu wa bunge jumapili iliyopita.

Waangalizi wa kimataifa walisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki,

Umoja wa Ulaya ni miongoni wa waliyotuma waangalizi wake kwenye uchaguzi huo.

Wakati ambapo tayari asilimia 94 ya kura zimeshahesabiwa, Rais Yushnko na mshirika wake wa chama cha mageuzi ya chungwa wanaoungwa mkono na nchi za magharibi Yulia Tymoshenko, wanaongoza wakiwa na asilimia 45.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo Viktor Yanukovych anayeungwa mkono na Urusi ana asilimia 34 ya kura.

Ukraine imefanya uchaguzi mara tatu toka mapinduzi ya chungwa mwaka 2004 ikiwa ni katika juhudi za kutafuta serikali imara.