1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiev.Rais kuunda serikali.

1 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBLE

Kiongozi wa upinzani nchini Ukraine Yulia Tymoshenko amesema anamtaka mshirika wake rais Viktor Yushchenko kuanza kuunda serikali mpya kuanzia leo Jumatatu. Hii inafuatia uchaguzi wa bunge ambapo chama cha kiongozi huyo wa upinzani kimeshinda kwa asilimia 32 ya kura katika hesabu ya mapema.

Chama cha rais kimepata asilimia 13.

Wakati huo huo , chama cha waziri mkuu Viktor Yanukovych kinaonekana kuwa kimepata kura nyingi zaidi katika uchaguzi huo wa bunge nchini Ukraine.