1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiev. Zoezi la kuhesabu kura karibu kumalizika.

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKw

Zoezi la kuhesabu kura katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili nchini Ukraine limefikia asilimia 89, na kuacha mvutano mkubwa baina ya vyama vinavyopendelea uhusiano na Russia na vile vinavyopendelea upande wa mataifa ya magharibi.

Tume ya uchaguzi wa Ukraine imesema kuwa chama cha waziri mkuu Viktor Yanukovych kinachounga mkono Russia kimepata hadi sasa asilimia 33.3. Wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea jana jumatatu wingi mdogo uliokuwa ukishikiliwa na kundi linalounga mkono mataifa ya magharibi la Yulia Tymoshenko uliyeyuka na kuliacha kundi hilo likiwa nyuma likiwa na asilimia 31.3. Rais Viktor Yushchenko ambaye ni mshirika wake ameamuru ufanyike uchunguzi kuhusiana na uwezekano wa kuwapo udanganyifu. Chama cha waziri mkuu cha Regions Party , pamoja na vyama vingine vitatu vidogo , huenda vikaunda muungano vikiwa na jumla ya asilimia 45.5. Vyama vya Tymoshenko na Yushchenko , ambavyo vilikuwa washirika katika mapinduzi wa mwaka 2004 ya rangi wa machungwa, vinaweza kupata asilimia 46.1 ya kura kwa mujibu wa takwimu za bunge. Baraza la Ulaya mjini Strassbourg limeitaka Ukraine kumaliza mzozo wake wa kisiasa .