KIEV : Putin aihakikishia Ukraine juu ya nishati | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KIEV : Putin aihakikishia Ukraine juu ya nishati

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameihakikishia Ukraine kwamba inaweza kuitegemea Urusi kwa usambazaji wa nishati.

Putin alikuwa akizungumza wakati wa ziara yake nchini Ukraine ambapo alikuwa na mazungumzo na Rais Viktor Yuschenko anayeungwa mkono na mataifa ya magharibi.Ukraine ni kituo muhimu cha kupitisha usambazaji wa gesi kutoka Urusi kuelekea Umoja wa Ulaya na mzozo wa gesi mwishoni mwa mwaka jana juu ya usambazaji wa gesi ya Urusi kwa Ukraine ulitibuwa usambazaji wa gesi kwa nchi kadhaa za Ulaya.

Ziara ya Putin nchini Ukraine ni ya kwanza tokea kutokea kwa kile kinachojulikana kama mapinduzi ya rangi ya chungwa miaka miwili iliopita na inafuatia kurudi tena madarakani kwa Waziri Mkuu anayeiunga mkono Urusi Viktor Yanukovych hapo mwezi wa Augusti.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com