1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiev. Makundi yote mawili yadai kupata ushindi.

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKd

Pande mbili hasimu katika uchaguzi wa bunge nchini Ukraine zimedai kupata ushindi wakati zoezi la kuhesabu kura linakaribia kufikia mwisho. Muungano unaounga mkono mataifa ya magharibi wa mapinduzi ya rangi ya chungwa unaoongozwa na rais Viktor Yushchenko na kiongozi wa upinzani Yulia Tymoshenko unaendelea kuongoza kwa wingi mdogo dhidi ya waziri mkuu anayeiunga mkono Russia Viktor yanukovich. Pande hizo mbili zinadai haki ya kuunda muungano utakaounda serikali katika bunge la nchi hiyo lenye wabunge 450. Chama cha Regions party cha waziri mkuu Yanukovich kinaongoza kikiwa na asilimia 34 ya kura na chama shirika cha kikomunist kina zaidi ya asilimia 5. Lakini jumla ya kura za muungano wa vuguvugu la machungwa zinafikia asilimia 45. Pande zote mbili zinashutumu upande mwingine kwa udanganyifu katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili.