1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KIEV: Maelfu waandamana kumpinga rais Yuschenko

Maelfu ya waandamanaji walimiminika kwenye barabara za mji mkuu wa Kiev nchini Ukraine kupinga agizo la rais Viktor Yuschenko la kulivunja bunge.

Wengi kati ya waandamanji hao walipeperusha vibendera vya rangi ya bluu ishara ya kukiunga mkono chama cha waziri mkuu Viktor Yanukovych.

Wakati huo huo wabunge wamekutana kukiuka amri ya rais Yuschenko ya kuvunjwa kwa bunge na kuitishwa uchaguzi wa mapema.

Rais Viktor Yuschenko na waziri wake mkuu wametumbukia katika mvutano wa kisiasa kwa muda wa mwezi mmoja sasa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com