1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Sudan yatetea uamuzi wa kumfukuza mwakilishi wa Umoja wa Mataifa

10 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBKJ

Serikali ya Sudan imetetea uamuzi wake wa kumfukuza mkuu wa Umoja wa Mataifa aliekuwa anaongoza uratibu wa masuala ya kibinadamu kusini mwa jimbo la Darfur.

Akifafanua uamuzi huo waziri wa sheria wa Sudan bwana Mohamed Ali al- Mardi amesema serikali ya nchi yake imemfukuza mwakilishi huyo al Haj Ibrahim kwa sababu ya kuwashauri wakimbizi kutorejea kwenye vijji vyao.

Waziri huyo amesema,kuwa viongozi katika jimbo la Darfur hawakuwa na njia nyingine ila kumfukuza mjumbe huyo ambae ni raia wa Canada.

Umoja wa mataifa umesema kufukuzwa mjumbe wake kutoka jimbo la Darfur kutazuia juhudi za kutoa msaada kwa watu wapatao milioni moja.