1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM.Muwakilishi wa umoja wa mataifa atakiwa kuondoka Sudan

Serikali ya Sudan imemtaka muwakilishi wa umoja wa mataifa nchini humo Jan Pronk aondoke katika muda wa siku tatu kutoka nchini humo.

Hatua hiyo imefuatia baada ya mwanadiplomasia huyo kuandika katika mtandao wake binafsi kwamba jeshi la Sudan limeshindwa nguvu mara mbili na waasi katika vita vya jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan katika miezi miwili iliyopita.

Pronk atarejea mjini New York kushauriana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan.

Sudan imekuwa ikipinga kupelekwa nchini humo wanajeshi 20,000 wa kimataifa wa kulinda amani.

Wanajeshi hao wa umoja wa mataifa wanatarajiwa kuchukuwa hatamu za kulinda amani kutoka kwa jeshi la umoja wa nchi za Afrika AU.

Takriban watu 200,000 wameuwawa na wengine milioni 2.5 wameyahama makaazi yao tangu vita vya mwaka 2003 katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com