1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Katibu mkuu wa umoja wa mataifa akutana na rais Bashir

6 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSG

Serikali ya Sudan imekubali kufanya mazungumzo mapya na waasi wa Sudan mwezi ujao wa Oktoba.

Hayo yamefahamishwa baada ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon kukutana na rais Omar El Bashier mjini Khartoum.

Mazaungumauzo hayo mapya yatafanyika nchini Libya tarehe 27 mwezi ujao na yanalenga kuyahusisha makundi yote ya waasi pamoja na yale yaliyokataa kutia saini makubaliano ya amani ya mwezi mei nchini Nigeria.

Serikali ya Sudan imekubali kutoa ushirikiano ili kufanikisha mazungumzo hayo na pia imesema itazingatia makubaliano ya kusimamisha mapigano katika jimbo la Darfur.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amesema kwamba ameweza kufikia maelewano na serikali ya mjini Khartoum juu pata hakikisho juu ya kupelekwa kikosi cha mchanganyiko cha kulinda amani cha wanajeshi 26,000 wa umoja wa mataifa na umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur.