1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM : Waasi wa zamani wadai kutekelezwa mkataba

17 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FE

Waasi wa zamani wa kusini mwa Sudan hapo jana wamedai vifungu viliobakia vya mkataba wa amani wa mwaka 2005 na serikali ya Khartoum vitekelezwe ifikapo tarehe 9 mwezi wa Januari ili kuyaokowa makubaliano hayo yaliokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya zaidi ya miaka 20.

Rais wa Sudan amekutana na ujumbe wa chama cha SPLM ukiongozwa na makao mwenyekiti wa chama hicho Riek Machar ukiwa ni mkutano wa kwanza tokea mawaziri wa SPLM kujitowa kwenye serikali hiyo mwezi uliopita.

Pande hizo mbili zimesema hazitorudi vitani lakini zimelaumiana kwa kushindwa kutekeleza mkataba huo.

Mwenyekiti wa SPLM Salva Kiir anatazamiwa kuwasili mjini Khartoum katika kipindi kisichozidi masaa 48 kuzungumza na Rais Omar Hassan al -Bashir na kutatuwa pingamizi hiyo.