KHARTOUM : Vikosi vya Afrika vya kutosha kwa Dafur | Habari za Ulimwengu | DW | 13.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM : Vikosi vya Afrika vya kutosha kwa Dafur

Mataifa ya Afrika yameahidi kutowa vikosi vya kutosha kulinda amani Dafur nchini Sudan kwa hiyo hakuna haja ya kuwahusisha wanajeshi kutoka nje ya bara hilo.

Alpha Oumar Konare mwenyekiti wa halmashauri ya Umoja wa Afrika amesema kutokana na ahadi walizopewa na mataifa ya Afrika hawatokuwa na haja ya kutumia wanajeshi wasio wa Afrika.

Konare amesema hayo baada ya kukutana na Rais wa Sudan Omar al Bashir mjini Khartoum hapo jana ambapo amesema wana wanajeshi wa kutosha wa Afrika kuwekwa kwenye jimbo la mizozo la magharibi mwa Sudan la Dafur.Ameongeza kusema kwamba kinachohitajika sasa ni fedha za kutosha kugharamia operesheni hiyo.

Umoja wa Mataifa hivi karibuni umeidhinisha uwekaji wa kikosi cha wanajeshi 26,000 mchanganyiko cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kulinda amani huko Dafur.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com