KHARTOUM: Serikali ya Sudan kukubali mpango mpya wa Umoja wa mataifa juu ya Darfur | Habari za Ulimwengu | DW | 18.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM: Serikali ya Sudan kukubali mpango mpya wa Umoja wa mataifa juu ya Darfur

Serikali ya Sudan ambayo inapinga kikosi cha kijeshi cha Umoja wa mataifa katika jimbo la Darfur, imeonekana kuunga mkono maridhiano juu ya kikosi cha kijeshi cha kulinda amani katika eneo lenye machafuko la Darfur, magharibi mwa Sudan. Mshauri mkuu wa rais wa Sudan, Omar el Bashir, amesema kuwa hakuna tatizo kwa kikosi cha mchanganyiko wakiwemo wanajeshi wa Umoja wa Afrika ambao tayari wako Darfur na ambao watapa vifaa kutoka kwa wafanyakazi wa Umoja wa mataifa. Mwishoe amezidi kusema mshauri wa rais wa Sudan, kikosi hicho kiwe na idadi kubwa ya wanajeshi kutoka Afrika na kuongozwa na Umoja wa Afrika.

Mpango huo mpya ulifikiwa mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kufuatia mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan.

Mratibu wa shughuli za kibinaadamu za Umoja wa mataifa, Jan Egeland, ambae alilitembelea eneo la Darfur, amesema mashambulizi dhidi ya raia yanayofanywa na wanamgambo bado yanaendelea karibu kila siku hata ndani ya kambi za wakimbizi. Umoja wa mataifa umesema, Jan Egeland, alilazimika kukatiza safari yake kwa kuwa serikali ya Sudan haikumuruhusu kuzitembelea baadhi ya sehemu za eneo hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com