KHARTOUM : Mkuu wa shughuli za binaadamu atimuliwa | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM : Mkuu wa shughuli za binaadamu atimuliwa

Maafisa wa serikali katika jimbo la kusini mwa Dafur nchini Sudan wamemtimuwa mkuu wa shughuli za kibinaadamu za Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa umesema Wael al- Haj- Ibrahim raia wa Canada ameshutumiwa kwa kukiuka sheria ambazo hazikutajwa.Ibrahim alikuwa akioongoza ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa Uratibu wa Masuala ya Kibinaadamu katika mji wa Nyale.

Ofisi hiyo inashughulikia msaada wa takriban watu milioni moja waliopotezewa makaazi yao.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amelezea waasi wake juu ya taathira za kutimuliwa kwa mkuu huyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com