1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Mauaji yaendelea Darfur, magharibi mwa Sudan

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCr6

Wachunguzi wa kimataifa na viongozi wa waasi nchini Sudan wanasema mapigano yameongezeka katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan. Kiongozi moja wa waasi amesema makumi ya watu waliuawa mnamo muda wa siku tatu zilizopita licha ya mapatano ya kusimamisha mapigano. Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya Umoja wa Afrika ambao majeshi yake yanasimamia amani katika jimbo lenye machafuko la Darfur, kuyashutumu majeshi ya serikali na wanamgambo wa Janjawid kuvunja mkataba wa usalama kwa kushambulia kwa ndege na kuvamia na majeshi ya nchi kavu. Waasi wametoa mwito kipelekwe kikosi cha kijeshi cha Umoja wa mataifa cha kulinda amani katika jimbo la Darfur, kikosi ambacho serikali ya Sudan imepikinga.