1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM : Kikosi cha Umoja wa Afrika kushambuliwa

Umoja wa Afrika umesema hapo jana ina taarifa kwamba kikosi chake huko Dafur kinaweza kuja kushambuliwa katika kipindi cha masaa 24 kutoka kwa waasi na wanachama wa kundi waliosaini makubaliano ya amani na serikali ya Sudan.

Hapo Jumatatu kundi jengine tafauti la wanamgambo liliingia El Fasher na kupambana na kundi la zamani la waasi liliosaini makubaliano ya amani na serikali hapo mwezi wa Mei.

Taarifa hiyo ya Umoja wa Afrika ambayo ina wanajeshi 7,000 huko Dafur imesema repoti zilizopokelewa na mapema zimedokeza kwamba mji wa El Fasher uko chini ya tishio la kushambuliwa katika kipindi kisichozidi masaa 24 na mmungano unaojumuisha kundi la SLA(M),G19 na NRF.

SLA(M) ni kitengo cha kijeshi cha kundi la SLA lililosaini makubaliano ya amani wakati G19 na NRF ni makundi ya waasi ambayo yameyakataa makubaliano hayo ya amani ya mwezi wa Mei.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com