1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum. Kijiji chateketezwa kwa moto.

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hc

Wachunguzi wa umoja wa mataifa wamesema kuwa kijiji kimoja katika jimbo lenye matatizo la Darfur nchini Sudan kimeharibiwa kwa kuchomwa moto, na kulazimisha watu kiasi cha 15,000 wakaazi wa eneo hilo kukimbia. Tukio hilo lilitokea katika makaazi ya haskanita, linafuatia mauaji ya wanajeshi 10 wa jeshi la kulinda amani la umoja wa Afrika Septemba 29 katika kituo cha karibu cha jeshi.

Kundi la waasi limesema kuwa kiasi cha watu 100 wameuwawa katika uharibifu huo, ambapo wanasema jeshi la Sudan lilihusika.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Sudan Lam Akol hata hivyo anatofautiana na taarifa hizi.

Jeshi la pamoja na umoja wa mataifa na umoja wa Afrika limethibitisha kuwa kijiji hicho kilikuwa chini ya udhibiti wa majeshi ya serikali.