KHARTOUM: Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ziarani Sudan | Habari za Ulimwengu | DW | 04.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM: Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ziarani Sudan

Kiongozi wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki-Moon amewasili nchini Sudan kwa ziara yake ya kwanza nchini humo kama Katibu Mkuu.Ni matumaini yake kuwa atasaidia kupata suluhisho kwa mgogoro wa Darfur,unaosemekana kuwa umesababisha vifo vya watu wapatao 200,000.

Azma ya ziara ya Ban Ki-Moon ni kuweka msingi wa majadiliano yanayotazamiwa kufanywa mwezi wa Oktoba,kati ya serikali ya Khartoum na viongozi wa makundi darzeni kadhaa ya waasi katika kanda hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com