1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya Zumwinkel

Oumilkher Hamidou22 Januari 2009

Meneja wa zamani wa shirika la Posta la Ujerumani afikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukwepa kulipa kodi ya mapato

https://p.dw.com/p/Ge8r
Aliyekua mkuu wa Posta Klaus ZumwinkelPicha: AP


Kesi dhidi ya mwenyekiti wa zamani wa shirika la Ujerumani la Posta,Deutschen Post,KIaus Zumwinkel inaanza leo katika mahakama ya mjini Bochum.Bwana huyo mwenye umri wa miaka 65 anatuhumiwa kukwepa kulipa kodi ya mapato yenye thamani ya mamilioni ya yuro.Kesi hiyo inatazamiwa kudumu siku mbili tuu,hasa kwasababu mtuhumiwa amekiri makosa yake na kurejesha serikalini fedha alizokwepa hapo awali kulipa.


Kuna maneno ambayo mtu huyatamka wakati wowote ule katika maisha yake,na kuna siku ambapo mtu anajuta kwamba aliwahi kutamka maneno kama yale.Tamko hili limetolewa na meneja mashuhuri Klaus Zumwinkel :


"Nimezaliwa katika jimbo la mto Rhine,nnafurahi kuishi katika jimbo la mto Rhine,nnajisikia vizuri sana na nnalipa kodi yangu ya mapato."


Matamshi hayo yaonyesha hayana ukweli hata kidogo.Kwasababu mwaka kama mmoja hivi uliopita,ilikua siku ya alkhamisi,february 14 mwaka 2008 muda mfupi baada ya saa moja ya asubuhi kengele ya mlangoni ililia katika nyumba ya Zumwinkel mjini Cologne.Walikua maafisa wanaowaandama watu wasiolipa kodi zao kama inavyotakikana.Dakika hiyo hiyo maafisa wenzao wakaingilia ofisi ya kiongozi huyo wa shirika la Posta,ghorofa ya juu kabisa ya makao makuu ya shirika hilo na kuanza kusachi.Siku moja baadae Zumwinkel akajiuzulu na kuachana pia na wadhifa wake wa mwenyekiti wa mabaraza ya usimamizi ya Telekom na Postbank.


Daraja aliyopanda meneja huyo mashuhuri kabisa nchini Ujerumani kufumba na kufumbua ikavunjika.


Zumwinkel,aliyejifunza ustadi wa kurekebisha na kuinua shughuli za kiuchumi kutoka shirika la ushaurinasaha la McKinsey,alipanda kilele mwa shirika kubwa kabisa la mawasili la ujerumasni-Deutsche Bundesport msimu wa mapukutiko mwaka 1989 na kufanikiwa kuipeleka Posta katika soko la hisa kwa jina "Faharasa ya njano" mnamo mwaka 2000.


Zumwinkel alitaka kwenda mbali zaidi,lengo likiwa kuligeuza shirika la Posta la Ujerumani likamate mstari wa mbele ulimwenguni.


"Unapoongoza shirika kubwa kama hili,sio kila mtu anaweza kufanikiwa mia bin mia.Lakini kwa jumla mtu anaweza kusema utaratibu wa kusawazisha hali ya mambo,umepita vizuri."


Sio kila kitu kimepita vizuri.Hivi sasa meneja huyo aliyekua akisifiwa kupita kiasi ,aliyetunukiwa nishani ya "ustahiki" ya shirikisho la jamhuri ya Ujerumani anabidi ajibu tuhuma za kuhamishia Lichtenstein,kodi ya mapato yenye thamani ya yuro laki 9 na 70 elfu,kati ya mwaka 2002 na 2006.Lakini kwakua kitita hicho kiko chini ya yuro milioni moja,Zumwinkel anatazamiwa kuhukumiwa kifungo cha nje tuu na pengine kumalizia maisha yake katika kasri alilolijenga Italy.

(Böhme,Henrik-DW Wirtschaft)