1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya maharamia inaburura miguu mjini Hamburg

23 Mei 2011

Katika muda wa nusu mwaka uliopita, ilianza kesi dhidi ya maharamia kumi wa Kisomali mjini Hamburg, lakini hadi sasa kesi hiyo haijafikia tamati. Mwendo ni wa kusua sua mno.

https://p.dw.com/p/11MH2
Baadhi ya maharamia kumi wa Kisomalia wakiwa mahakamani mjini Hamburg miezi saba baada ya kuivamia na kutaka kuiteka nyara meli ya MS "Taipan"Picha: dapd

Katika muda wa nusu mwaka uliopita ilianza mjini Hamburg kesi dhidi ya maharamia kumi wa Kisomali. Shtaka lao ni kwamba watu hao waliiteka nyara meli moja ya Ujerumani inayojulikana kama "Taipan" ,katika eneo la bahari katika pembe ya Afrika na kudai malipo. Shauku ya vyombo vya habari ilikuwa kubwa mno, kwamba kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 400 , maharamia wamepelekwa mbele ya mahakama nchini Ujerumani. Tangu wakati huo, lakini, shauku hiyo imeporomoka, na wengi wa wachunguzi wanaona kuwa kesi hiyo maarufu imekuwa ndefu mno bila sababu.

Kwa muda wa siku 33 wa kuendeshwa kesi hiyo, hali inaonekana kuwa ile ile. Katika chumba cha mahakama namba 337 katika mahakama mjini Hamburg ,wako washtakiwa hao kumi kutoka Somalia. Bila wasi wasi kila mshtakiwa huweka sawa kiti chake, humsalimu wakili wao kwa muda mfupi na kuvalia chombo cha kusikiliza masikioni.

Kila kitu tangu nusu mwaka uliopita katika chumba hicho cha mahakama , kinatafsiriwa ili watu hawa waweze kukielewa kupitia chombo hicho cha kusikilizia masikioni , wataalamu wa uchunguzi sita hadi sasa wamekwisha toa taarifa zao na mashahidi 11 watasikilizwa. Na pia wataitwa maafisa kadha pamoja na waendesha mashtaka kwa upande wa utetezi. Baada ya kusikilizwa madai ya msingi kesi hiyo baada ya miezi miwili itakuwa imemalizika. Lakini hadi miezi sita sasa tangu kuanza kwa kesi hiyo bado mwisho wake hauonekani.

Gabriele Heinecke ni wakili wa baadhi ya washtakiwa wa uharamia. Na kwake yeye pia hali ya uvumilivu inaanza kumwishia.

Kwa kweli ni hali yenye changamoto kubwa kwa mahakama hapa, katika kuweka kila kitu katika utaratibu, nani amefanya nini. Hali hiyo imechukua muda mrefu, na hii ni sawa. Lakini suala kuu hapa ni kwamba ni kitu gani kilichowashawishi watu hawa kumi kuingia katika meli ya Taipan, suala hili hadi sasa halijazungumziwa. Tunaelekea katika suala hilo kwa taratibu mno.

Kuna swali , ambalo linaweza kusaidia kutoa uamuzi; Ni nini kilichosababisha Wasomali hawa , kuyaweka maisha yao katika hatari na kuteka nyara meli. Na kuweza kujibu swali hili, ni lazima lifahamike suala la mazingira ya kimaisha ya vijana hawa kumi wa Kisomali. Ni umasikini kiasi gani ulikuwa unawakabili? Ni kiasi gani walikuwa na hali ya kukata tamaa. Kuna matumizi ya nguvu ya kiasi gani katika maisha ya kila siku nchini mwao.

Deutschland Somalia Prozessauftakt gegen Piraten in Hamburg
Mshatakiwa wa Kisomali akiwa mahakamani pamoja na mawakili wa maharamia hao.Picha: dapd

Kazi waliyopewa wachunguzi wa mambo kama haya inatoa nguvu kubwa , ya kuonyesha picha ya hali halisi nchini Somalia. Kwa msaada wa picha kadha zilizooneshwa mahakamani, mtaalamu wa masuala ya Somalia , Volker Matthies, amejaribu kuelezea hali ya mfumo wa koo , pamoja na muundo wa utawala wa nchi hiyo. Pamoja na hayo baadhi ya maswali ya mawakili, hakuweza kuyapatia majibu. Kwa msingi wa hali ya usalama mtaalamu huyo wa masuala ya kisiasa hakuweza kukaa katika eneo hilo kwa muda wa miaka kadha.

Ni kitu kinachoeleweka kwamba kutokana na hali ngumu ya mapigano pamoja na kuporomoka kwa mfumo wa utawala ni vigumu kupata takwimu sahihi zenye kuaminika.

Mwandishi : Jan-Philipp Scholz / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Othman Miraj.