Kesi hii si sawa | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kesi hii si sawa

Ameungama kupanga mashambulio ya Septemba 11 2001 kuanzia mwanzo hadi mwisho – hiyo ndiyo sentensi muhimu zaidi katika taarifa yake Sheikh Mohammed, mfungwa wa gereza la Guantanamo. Taarifa hizo za mahojiano aliyoyafanyiwa Sheikh Mohammed, mtuhumiwa aliyeungama pia alikuwa dhamana wa njama nyingine nyingi za kigaidi, ilichapishwa na serikali ya Marekani. Haijulikani ikiwa mahojiano haya yalifanywa kwa kutumia mateso. Katika taarifa zilizochapishwa kuna tetesi fulani za matumizi ya mateso. Ufuatao ni uchumbuzi wa Peter Philipp.

default

Khalid Sheikh Mohamed ni mmoja kati ya watuhumiwa 14 muhimu zaidi kwenye orodha ya washirika wa kundi la kigaidi la “Al-Kaida” wanaotafutwa na Marekani. Akiwafuata Osama Bin Laden na Ayman al Zawahiri, Sheihk Mohamed anaaminika alichukua nafasi ya tatu katika “Al-Kaida”. Lakini baada ya kukamatwa nchini Pakistan miaka minne iliyopita na kupelekwa kwa idara za Kimarekani hakuna habari zaidi Sheikh Mohamed alipelekwa wapi na wapi. Inasemekana kuwa hadi mwaka ulipita alifungwa katika gereza fulani la CIA, idara ya ujasusi ya Marekani, ambalo limekosolewa vikali hivi karibuni, na halafu kupelekwa Guantanamo. Huko kulipatikana habari ya kwamba Sheikh Mohamed aliungama kuwa dhama wa operesheni nzima ya mashambulio ya Septemba 9, 2001 nchini Marekani pamoja na hujuma nyengine zilizofungamanishwa na mtandao wa Al Kaida.

Taarifa hizo zinaifaa serikali ya Marekani. Duniani nzima kuna ukosoaji mkali dhidi ya magereza ya CIA na la Guantanamo na mpaka sasa Marekani ilikuwa na hoja chache kuzima kukosolewa huko. Jinsi walivyowatendea watuhumiwa wa ugaidi ilikuwa dhidi ya sheria za kimataifa. Na si mara moja tu kwamba iligunduliwa kuwa wafungwa fulani wamekamatwa bila ya hatia. Hata hivyo hawakuruhusiwa kuwa na wakili au kuwa na fursa yoyote kuachiliwa huru – isipokuwa tu Marekani haikuwa na maslahi naye – kama katika kesi ya Mjerumani wa asili ya kituruki Murat Kurnaz.

Kesi ya Sheikh Mohamed lakini ni tofauti. Ni mara ya kwanza mtuhumiwa kuungama wazi. Basi ni fursa nzuri kwa serikali ya Washington kulitetea gereza la Guantanamo. Kwa hivyo hakuna huruma kwa gaidi aliyesababisha mamia ya watu kuuawa. Inaonekana kama Marekani ina matumaini kuwa kuungama la Khalid Sheikh Mohamed kutatuliza wakosoaji wake.

Lakini matumaini haya hayatatimizwa. Kwa sababu hata mtu kama Khalid Sheikh Mohamed anafaa kufikishwe mbele ya mahakama ya halali na kufanyiwa kesi. Si sawa kesi yake kusikilizwa na kamati ya faragharani. Kwa mujibu wa yale yanayojulikana juu ya jela la Guantanamo, kimsingi inaaminika kuwa wafungwa huteswa. Kwa hivyo ni kinyume na sheria.

Suali ikiwa Sheikh Mohamed aliteswa au la na ikiwa kuungama kwake kulazimishwa halitajibiwa na ofisi za serikali. Lakini inajulikana kwamba Washington haiwadekezi wafungwa.

Bila shaka, lazima gaidi kama Sheikh Mohamed wazuiliwe na waadhibiwe. Lakini kwa njia ya kisheria. Katika kesi hiyo, hata hivyo, kuna mashaka juu ya hayo.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com