1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenyatta na Ruto kuwania urais Kenya

3 Desemba 2012

Wanasiasa wawili wa Kenya wanaowania wadhifa wa urais na ambao wameshtakiwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa uchochezi wa ghasia, wamesema wanajiunga pamoja kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mwakani.

https://p.dw.com/p/16ufg
epa02623841 (FILE) A file photo dated 15 December 2010 shows Kenya's Finance Minister and Deputy Prime Minister Uhuru Kenyatta arriving at a press conference on the day the International Criminal Court (ICC) announced six prominent Kenyans, which included Kenyatta, who are said to be responsible for masterminding the country's 2007/08 post-election violence that left some 1,300 dead. According to a local report, five suspects, Kenyatta, former higher education minister William Ruto, suspended Industrialisation Minister Henry Kosgey, former police commissioner Maj-Gen Hussein Ali, and Head of Operation at KASS FM radio Joshua Arap Sang said on 09 March 2011 that they will honor summonses issued for the charges of crimes against humanity by the pre-trial chamber of the ICC. The sixth suspect is the Secretary to the Cabinet and Head of the Civil Service Francis Muthaura. EPA/DAI KUROKAWA
Kenia Uhuru KenyattaPicha: picture-alliance/dpa

Kwa uamuzi huo Kenya inakabiliwa na hatari ya kuwa na viongozi ambao wanakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita mbele ya mahakama ya kimataifa mjini The Hague.

Makamu waziri mkuu Uhuru Kenyatta, mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya baada ya uhuru kutoka Uingereza, atawania kiti cha urais wakati waziri wa zamani William Ruto anamatumaini ya kuwa makamu rais, kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Former Kenyan Education Minister William Samoei Ruto sits in the courtroom of the International Criminal Court (ICC) in The Hague, Netherlands, Thursday, Sept. 1, 2011. Ruto is one of three senior Kenyan leaders appearing at the International Criminal Court for a hearing at which judges will decide whether evidence against them is strong enough to merit putting them on trial on charges of orchestrating deadly violence in the aftermath of disputed 2007 elections. (AP Photo/Bas Czerwinski)
William Samoei RutoPicha: AP

Uchaguzi huo utakuwa wa kwanza chini ya katiba mpya na wa kwanza tangu uchaguzi wa mwaka 2007 ambao umesababisha ghasia na zaidi ya watu 1,200 wameuwawa. Kenya hapo kabla imekuwa pepo ya utulivu katika eneo ambalo limekuwa likikumbwa na matatizo.

Mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague imesema mwezi Julai kuwa Wakenya wanne maarufu , ikiwa ni pamoja na Kenyatta na Ruto, watafikishwa mahakamani kwa madai ya kuhusika katika uchochezi wa ghasia zilizosababisha umwagikaji wa damu.

Kenyans of African and Asian Communities wait in a line to vote at Westlands Primary School, Nairobi, Kenya, Friday, Dec. 27, 2002, in a nationwide election in which more than 10.5 million voters are expected to participate. Uhuru Kenyatta, Mwai Kibaki, Simeon Nyachae, James Orengo and David Waweru Ng'ethe are running for the president, but they also have to win their parliamentary seats as well. (AP Photo/Sayyid Azim)
Wapiga kura wakisubiri kupiga kura katika uchaguzi uliopita 2007Picha: AP

Wote wanakana madai hayo.

Kuna hofu kuwa Kenya inaweza kukabiliwa na mkwamo wa kisiasa ama vikwazo vya kiuchumi kutoka mataifa ya magharibi iwapo watu hao watakaidi kufika katika mahakama ya ICC.

"Tumekubaliana kuwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, mwaka ujao chama cha URP na TNA vitaungana na kuunda serikali mpya," Ruto amewaambia maelfu ya wafuasi wao katika mkutano wa hadhara wa makundi hayo ya United Republican Party na National Alliance Party cha Kenyatta katika mji wa Nakuru katika jimbo la Rift Valley, kilometa 140 kaskazini magharibi ya mji mkuu Nairobi.

Mawaziri wanane na wabunge kadha walikuwapo katika mkutano huo.

Hofu

Mahakama ya ICC imepanga kesi hizo za uhalifu dhidi ya ubinadamu zisikilizwe mwezi Aprili , mwakani , mwezi mmoja baada ya uchaguzi wa rais katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa katika Afrika mashariki.

Hatua ya Ruto na Kenyatta kuungana kuwania urais nchini Kenya , inaleta uwezekano wa kuwa na rais ambaye ameshtakiwa katika mahakama ya ICC mjini The Hague.

Shirika la kijamii lapinga

Shrika la kijamii nchini Kenya linalojulikana kama International Centre for peace and conflict, taasisi inayoshughulikia uchunguzi wa amani na mizozo imefungua mashtaka siku ya Ijumaa katika mahakama kuu ya kenya kupinga uwezekano wa Ruto na Kenyatta kuwania madaraka ya kuchaguliwa, kutokana na kesi yao mjini The Hague.

Kesi hiyo imefunguliwa baada ya kesi kama hiyo kuondolewa mahakamani.

Ivory Coast opposition leader Alassane Ouattara, left, looks on as Kenyan Prime Minister Raila Odinga speaks to the press at the Golf Hotel in Abidjan, Ivory Coast, Monday, Jan. 3, 2011. African leaders on Monday were offering Laurent Gbagbo an amnesty deal on condition he cedes the presidency peacefully to Ouattara, the internationally recognized winner of Ivory Coast's elections, an official said Monday. (Foto:Emanuel Ekra/AP/dapd)
Waziri mkuu wa Kenya Raila OdingaPicha: AP

Uchunguzi wa maoni mwezi Oktoba yameonyesha kuwa karibu robo ya Wakenya wanatarajia uchaguzi wa rais mwezi Machi kuchafuliwa na ghasia za baada ya uchaguzi huo.

Viongozi hao wawili wataingia katika kinyang'anyiro hicho cha urais wakipambana na waziri mkuu Raila Odinga kutoka chama cha Orange Democratic Movement, miongoni mwa wagombea wengine.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Yusuf Saumu