1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenyatta athibitishwa kuwa mshindi wa urais Kenya

30 Machi 2013

Mahakama ya Juu ya Kenya leo imekubaliana kwa kauli moja kuwa Uhuru Muigai Kenyatta ndiye rais halali wa Kenya, pamoja na mgombea mwenza wake William Ruto

https://p.dw.com/p/187Es
A general view shows the proceedings at the Supreme Court in Kenya's capital Nairobi March 30, 2013. Kenya's Supreme Court ruled on Saturday Uhuru Kenyatta was elected president fairly, unanimously rejecting a challenge from defeated candidate Raila Odinga that the vote was marred by rigging and technical problems. REUTERS/Noor Khamis (KENYA - Tags: POLITICS ELECTIONS)
Kenia Supreme Court Gerichtssaal Urteil technische Probleme Wahlergebnis PräsidentschaftswahlenPicha: Reuters

Jaji Mkuu Willy Mutunga amesema Kenyatta na Ruto walichaguliwa kwa njia halali. Mahakama hiyo imeamuru kuwa uchaguzi mkuu wa Machi 4 ulifanywa kwa njia ya huru, haki na halali.

Kenyatta anatarajiwa kuapishwa mnamo Aprili 9. Atakuwa rais wa nne wa Kenya tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka kwa Uingereza miaka 50 iliyopita. Babake Mzee Jomo Kenyatta alikuwa rais wa kwanza wa Kenya kabla y akifo chake mwaka wa 1978.

Uhuru Kenyatta ataapishwa rasmi Aprili 9 jijini Nairobi
Uhuru Kenyatta ataapishwa rasmi Aprili 9 jijini NairobiPicha: REUTERS

Raila akiri kushindwa

kizungumza muda mfupi baada ya kutolewa huku hiyo, Waziri Mkuu Raila Odinga amekiri kushindwa, akiwatakia kila la kheri Kenyatta na Ruto wanapojianda akuendesha serikali mpya.

Mahakama imepinga ombi la mpinzani wake Raila Odinga la kuwepo hila katika uchaguzi huo. Kenyatta na Ruto wanakabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC ya kuhusika katika mchafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007 nchini Kenya.

Kenyatta mwenye umri wa miaka 51, alipata zaidi ya kura milioni 6.13, ikilinganishwa na zile za Odinga milioni 5.3 ambapo kulikuwa na kubwa ya wapiga kura kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.

Takribani wakenya milioni 14.3 walijisajili kama wapiga kura na zaidi ya kura milioni 12.3 zikapigwa. Takribani nusu ya Wakenya milioni 43 wako chini ya umri wa umri wa miaka 18.

Waziri Mkuu Raila Odinga ameahidi kuendeleza harakati za kutaka mageuzi Kenya baada ya kushindwa
Waziri Mkuu Raila Odinga ameahidi kuendeleza harakati za kutaka mageuzi Kenya baada ya kushindwaPicha: Reuters

Huu ulikuwa uchaguzi wa kwanza tangu ule wa Desemba mwaka wa 2007 kusababisha ghasia za kikabila, ambapo takribani watu 1,000 waliuawa na mamia ya maelfu wakawachwa bila makaazi.

Serikali ya muungano kisha iliundwa miezi michache baadaye kufuatia juhudi za jamii ya kimataifa. Katiba mpya ikaidhinishwa nchini humo mwaka wa 2010. Kesi hiyo imeonekana kuwa mtihani wa kwanza uliofana kuhusiana na demokrasia, ambayo iliimarishwa na katiba mpya.

Uingereza yampongeza Kenyatta

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amewataka Wakenya kukubali uamuzi huo wa mahakama ya juu, wakati akimpongeza Uhuru Kenyatta kwa kushinda uchaguzi wa rais.

Cameron amewataka Wakenya kujivunia ishara waliyotuma kote ulimwenguni kuhusiana na kujitolea kwao kupiga kura kwa wingi kama haki yao ya kidemokrasia.

Wkati huo huo, polisi wamelazimika kufyatua mabomu ya kutoa machozi wakati mamia ya vijana walipofanya maandamano mjini Kisumu. Vijana hao walikuwa wakirusha mawe na kusema “Hakuna Raila, Hakuna amani”.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA

Mhariri: Josephat Charo