Kenya: Waziri wa zamani wa Ulinzi Njenga Karume afariki | Matukio ya Afrika | DW | 24.02.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Kenya: Waziri wa zamani wa Ulinzi Njenga Karume afariki

Waziri wa zamani wa Ulinzi nchini Kenya Njenga Karume amefariki dunia hii leo asubuhi mjini Nairobi baada ya kuugua saratani.

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amempoteza rafiki yake wa karibu

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amempoteza rafiki yake wa karibu

Marehemu Karume amefariki akiwa na miaka 83. Rais Mwai Kibaki ametoa salamu zake za rambi rambi kwa jamaa wa familia ya Marehemu huku akisema amempoteza rafiki yake wa karibu.

Amina Abubakar amezungumza na Martin Shikuku ambaye ni mwanasiasa mkongwe na kwanza anaelezea jinsi alivyoipokea taarifa ya kifo cha marehemu Njenga Karume.

(Kuskiliza makala hii, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Abdulrahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada