1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kushiriki awamu ya tatu ya chanjo ya Malaria

Lilian Mtono
26 Aprili 2021

Kenya inatarajiwa kushirkishwa kwenye awamu ya tatu ya majaribio ya chanjo ya malaria kwa lengo la kuboresha juhudi za taifa hilo za kukabiliana na ugonjwa huo.

https://p.dw.com/p/3saS6
Malaria-Bekämpfung in Afrika | Kenia | Impfstoff Mosquirix
Picha: Brian ONGORO/AFP

Kwenye awamu ya pili ya jaribio hilo lililofanyikia nchini Burkina Faso, chanjo hiyo ilionesha ufanisi wa asilimia 77, kwa watoto 450 waliokuwa na kati ya umri wa miaka mitano na miezi 15. Majaribio hayo yalifanyika kwa kipindi cha miezi 12.

soma zaidi: WHO: Mapambano ya malaria yanakwamishwa na COVID-19, fedha

Awamu ya tatu itawajumuisha watoto 4,800 walio na umri chini ya miaka mitatu.

Mataifa mengine ambayo yatashirikishwa kwenye awamu ya tatu ya majaribio hayo ni pamoja na Tanzania, Mali na Burkina Faso.

Chanjo hiyo ilitengezewa katika Chuo Kikuu cha Oxford kilichoko Uingereza na Taasisi ya Chanjo iliyoko India.