KENNEBUNKPORT: Rais Bush kushirikiana na rais Putin kuutanzua mzozo wa Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 03.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KENNEBUNKPORT: Rais Bush kushirikiana na rais Putin kuutanzua mzozo wa Iran

Rais Geroge W Bush wa Marekani na rais Vladamir Putin wa Urusi wamekubaliana kushirikiana kuutanzua mzozo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Katika mazungumzo yao mjini Kennebunkport, rais Bush amesema rais Putin anaunga mkono kutuma ujumbe mkali kwa Iran kupitia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Viongozi hao lakini hawakukubaliana mengi kuhusu mpango wa Marekani kutaka kujenga mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora mashariki mwa Ulaya.

Rais Putin amewaambia waandishi wa habari katika shamba la familia ya rais Bush huko Kennebunkport, Maine, kwamba upanuzi wa washirika wa Ulaya itakuwa njia ya kulitatua swala hilo.

Urusi inapinga juhudi za Marekani kujenga mifumo ya rada na ya ulinzi nchini Poland na jamhuri ya Ucheki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com