1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kelvin Ruud ni waziri mkuu mpya wa Australia

Josephat Charo24 Novemba 2007

Waziri mkuu wa Australia, John Howard, ameshindwa na kiongoziwa chama chamacha Labour, Kelvin Ruud. Bwana Howard huenda asichaguliwe katika eneo analoliwakilisha bungeni.

https://p.dw.com/p/CSl6
John Howard akiwa amesimama karibu na bango la picha ya Kelvin Ruud (kushoto)Picha: AP

Kiongozi wa chama chama Labour nchini Australia, Kevin Ruud, ameshinda uchaguzi hii leo hivyo kuumaliza utawala wa miaka 11 wa waziri mkuu John Howard.

Bwana Howard amekubali ushindi wa chama cha Labour. Amesema, ´Muda mfupi uliopita nimepigia siku bwana Kelvin Riuud na kumpongeza pamojana chamacha Labour kwa ushindi wake mkubwa.´

Kelvin Ruud amesema ameukubali ushindi na kusema Australia imeangalia siku za usoni, wakati alipotoa hotuba yake ya ushindi mjini Brisbane katika jimbo la Queensland, iliyoonyeshwa moja kwa moja katika televisheni nchini kote.

Kelvin Ruud amesema wakati umewadia kuandika ukurasa mpya katika historia ya Australia.

Ushindi wa kiongozi huyo, ulioshangiliwa kwa vishindo na wafuasi wake umemuabisha waziri mkuu anayeondoka, John Howard wa chama cha kiliberali.

Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi ya Australia yamedhihirisha chama cha Labour kimeshinda kwa asilimia 53 wakati asilimia 70 ya kura zilipokuwa zimehasabiwa. Chama cha John Howard kimejipatia asilimia 46.7 ya kura hizo.

John Howard amezungumza kwa njia ya simu na Kevin Ruud na kumpongeza kwa ushindi wake. Howard huenda asichaguliwe tena katika eneo analoliwakilisha bungeni.