Matukio ya Kisiasa
Katibu wa tume ya uchaguzi wa chama cha CUF ziarani katika nchi za Skandinavia
Katibu wa Tume ya Uchaguzi ya Chama cha CUF huko Tanzania, Muhene Said Rashid, anazitembelea nchi za Skandinavia za Finland, Sweden na Denmark.
Anajaribu kuzihimiza nchi hizo, hasa kwa vile Sweden hivi sasa ni rais wa Umoja wa Ulaya, ziweke ushawishi wao kuona kwamba watu wote walio na haki ya kupiga kura huko Zanzibar wanapata haki hiyo bila ya kuwekewa vizuizi. Othman Miraji amezungumza kwa njia ya simu na Muhene Said Rashid alipokuweko Stockholm, mji mkuu wa Sweden, na mjumbe huyo alikua na haya ya kueleza. Mtayarishaji: Othman Miraji Mhariri: Mohamed Abdulrahman
Sauti na Vidio Kuhusu Mada
Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa
Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com