Katiba ya Ujerumani - Miaka 58 | Matukio ya Kisiasa | DW | 23.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Katiba ya Ujerumani - Miaka 58

Katiba ya Ujerumani ilitangazwa tarehe 23 mwezi Mei mwaka 1949 na inaendelea kutumika hadi hii leo. Lakini hivi karibuni,kumekuwepo midahalo juu ya suala kama mageuzi fulani yapaswa kufanywa kuambatana na hali mpya kisiasa iliopo hivi sasa.

Kansela wa kwanza wa Ujerumani Adenauer akitia saini katiba ya Ujerumani

Kansela wa kwanza wa Ujerumani Adenauer akitia saini katiba ya Ujerumani

Kikao cha mwanzo cha bunge la Ujerumani kilipofunguliwa tarehe mosi Septemba mwaka 1948,Waziri mkuu wa jimbo la North-Rhein-Westfalia,wakati huo,Karl Arnhold alieleza jukumu muhimu kabisa la wabunge 65.Wao walikuwa na jukumu la kutayarisha katiba ya nchi ambayo Wajerumani wataweza kujitambulisha nayo,baada ya Vita Vikuu vya pili.Alieleza jukumu hilo kwa kusema hivi:

“Katiba hiyo iwe waraka wa uhai wa umma wa Kijerumani.Katiba hiyo impe kila mmoja imani na kumuhakikishia kuwa haki ya binadamu itadhaminiwa na kulindwa na taifa kwa kila njia.Vile vile ihakikishe kuwa kila mmoja anaweza kuishi na kufanywa kazi kwa uhuru bila ya kuhofia maisha yake.”

Wakati huo huo,Konrad Adenauer ambae baadae alikuja kuwa Kansela wa kwanza wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani,hapo tarehe mosi Septemba mwaka 1948 alisisitiza kuwa bunge linapaswa kufanya kazi zake kwa uhuru na bila ya kuingiliwa.Lakini kulikuwepo vikwazo katika katiba iliyoandaliwa na madola shirika.Katiba hiyo kwa kweli haikuitwa katiba,ili iweze kueleza waziwazi mfumo wake wa mpito,lakini hali ya mambo ikabadilika baada ya Ujerumani kutengwa sehemu ya Magharibi na Mashariki kufuatia vita baridi. Madola shirika yalitaka kuhakikisha kuwa katiba itatia maanani makosa ya katiba ya Jamhuri ya Weimar,katiba ambayo ilirahisiha kuvamia madola mengine au hata kuruhusu kufanya hivyo. Konrad akaeleza hivi:

“Ujerumani binafsi haina uwezo wa kisiasa. Imegawika sehemu mbili.Tunatekeleza wajibu wetu kwa kuamini lengo letu kwa dhati kwamba kwa njia hii,siku moja tutafanikiwa kuwa na muungano wa Ujerumani nzima.”

Shabaha ya kuiunganisha Ujerumani ilitajwa katika utangulizi na katiba yenyewe,ili lengo hilo liweze kupatiwa katiba ya taifa lililoungana.

Vipengele 19 vya kwanza ni kiini cha katiba, vikihusika na haki za binadamu na raia.Ukweli kuwa haki hizo zimetangulizwa katika katiba huonyesha umuhimu wake.Haki ya kimsingi ya katiba si lengo tu la taifa,bali haki hiyo,haipaswi kuguswa.

Katiba haikuandikwa upya hata baada ya kupatikana muungano wa Ujerumani mwaka 1989.Baadhi ya wananchi wanahisi kuwa si Wajerumani wa Mashariki tu bali Wajerumani wote wamenyimwa nafasi ya kutoa mchango wao katika katiba mpya.Kwa upande mwingine,wapo wanaosema,katiba ya hivi sasa ni mfano wenye ufanifu na hakuna hata haja ya kuibadilisha katiba hiyo.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com